7 Aprili 2013 - 19:30
Mahakama ya Misri Kuchunguza tuhuma dhidi ya Mursiy

Mahakama ya Misri imetoa hukumu ya kuchunguzwa faili la mashtaka dhidi ya Rais wa jamhuri ya Misri ambaye ni kutoka katika kikundi cha wenye fikra za kiislamu

Shirika la habari la AhlulBayt(a.s)- ABNA; moja kati ya vyanzo vya kisheria ya Misri imetangaza kuwa, mahakama kuu ya Misri imetoa hukumu ya kufuatiliwa na kuchunguzwa faili la mashtaka dhidi ya Rais wa jamhuri ya Misri.Kwamujibu wa ripoti hii (Abul Ula Madhiy) mkuu wa kikundi cha(Al wasat) amedai kuwa Mursiy katika baadhi ya mazungumzo yake alisema, wizara ya masuala ya mawasiliano ya Misri katika mwaka ulipita kuwa ilikusanya mamia ya wahalifu ambapo elfu nane kati yao wako mjini Cairo.Yasemekana maneno hayo aliyassema ktika hutuba yake akiwa na wafuasi na wanachama wa kikundi chakeییی nakuongezea kuwa matukio ya kinyama yaliotokea hivi karibu katika nchi hiyo wizara ya mawasiliano inahusika.Kwa sababu ya tuhuma hizo Abdul Rahman Al Aqariy ameyafikisha mashtaka hayo katika mahakama kuu ya Misri.Hii ni katika hali ambayo ofisi ya Rais mjini Cairo imekanusha tuhuma hiyo. Mkuu wa Mahama kuu ya Misri ambaye amepewa mamlaka hayo na Mursiy alipinga mashtaka hayo ama baadae alilikabidhi faili hilo kati ya moja ya mahakama ya nchi hiyo ili kufanya uchunguzi zaidi.